ZOEZI LA UCHUKUAJI FOMU YANGA LADODA

ZOEZI la uchukuaji fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika klabu ya Yanga limedoda baada ya wanachama wachache kujitokweza.
Zoezi hilo lililoanza juzi hadi kufikia mchana wa leo ni wagombea sita tu ndio waliojitokeza kuchukua fomu hizo ambapo kati yao ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa kamati ya utendaji.
Zoezi hilo litakomea juni 6 kabla ya uchaguzi huo ambao ni wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi ukipangwa kufanyika Julai 15.

Comments