YONDAN NUSURA ATIMULIWE STARS, TFF YAGOMA KUZUNGUMZIA SAKATA LAKE

BEKI wa kati wa timu ya Simba Kelvin Yondan nusura atimuliwe katika kambi ya timu ya Taifa baada ya kutoroka na kwenda kusaini mkataba na klabu ya Yanga.
Habari kutoka kambi ya Stars iliyopo hoteli ya Tansoma katikati ya jiji la Dar es Salaam zinaeleza kuwa kocha mkuu wa Stars Kim Poulsen alimuweka kiti moto nyota huyo baada ya kubaini kuwa hakuwepo kambini usiku wa juzi, lakini baada ya kujitetea ndipo alipoamua kumsamehe.
Uongozi wa Simba kupitia mwenyekiti wake Alhaj Ismail Aden Rage umesisirtiza kuwa Yondan ni mchezaji wake halali na kwamba Yanga wamebugi step kumsainisha mkataba mptya.
Kama hiyo haitoshi, Rage alisema wanatarajiwa kufikisha suala hilo kwa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) na lile la Kimataifa (FIFA) kwani hata mkataba wenyewe huo una utata katika baadhi ya vipengele, huku kiongozi aliyeshiriki kusimamia zoezi hilo si kiongozi halali wa Yanga.
Huku hayo yakiendelea, TFF kupitia kwa msemaji wake Boniface Wambura imeshindwa kuzungumzia juu ya sakata hilo na kuombwa lipewe nmuda kwanza ya kutafuta vielelezo kuhusina na mchezaji huyo ambaye amelamba kitita cha shilingi mil.30 kwa ajili ya kumwaga wino Yanga ambapo pia atakuwa akilambva mshahara wa sh.800,000 kwa mwezi.