WANAWAKE WENYE SIFA NA VIGEZO WAITWA YANGA

WAKATI zoezi la uchukuaji na urejeshaji fom,u za kuwania uongozi katika klabu ya Yanga likimalizika kesho, kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo imewaita wanawake wenye sifa na vigezo kujitosa kuwania uongozi.
Wito huo umetolewa na katibu wa kamati hiyo, Francis Kaswahili alipokuwa akizuzungumzia zoezi la uchukuaji fomu na kusema kwamba anasikitishwa na jinsia hiyo kutojitokeza mpaka sasa.
"Kwa kweli ni jambo la kusikitisha sana, yaani Yanga ni klabu kubwa na yenye wanachama wa kila rika lakini nashangazwa mpaka sasa hakuna jinsia ya kike iliyojitokeza kuchukua fomu...jamani waandishi wahamasisheni kina mama wajitokeze,"alisema.
Aidha, Kaswahili aliongeza kuwa mpaka sasa wagombea 19 wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi utakaofanyika Julai 15.

Comments