UTATA WATAWALA KUACHWA KWA BOBAN

UTATA umetawala kuhusiana na kuachwa katika safari ya Ivory Coast kwa  mshambuliaji wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' Haruna Moshi 'Boban'.
Boban na Nassor Masoud Cholo waote kutoka klabu ya Simba wameachwa katika safari hiyo baada ya kugundulika kuwa majeruhi saa chache kabla ya kuondoka.
Kocha Mkuu wa Stars Kim Poulsen alisema kwamba wachezaji hao walibainika kuwa na maumivu ya muda mrefu hivyo wanahitaji matitabu.
Hata hivyo taarifa nyingine zinaeleza kwamba Boban ameachwa kutokana na tatizo la pasi ya kusafiria kwani inadaiwa hata alipokwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwenye mazishi ya aliyekuwa mchezaji wa Simba Patrick Mafisango alitumia pasi ya muda.
Lakini TFF kupitia kwa katibu wake Mkuu Angetile Osiah imesisitiza kuwa Boban ameachwa kutokana na kuwa majeruhi na si vinginevyo.
"kama alienda DRC kwa pasi ya makaratasi ni suala la Simba lakini TFF tunajua amebaki sababu ya kuwa majeruhi,"alisema Osiah.
Mbali na nyota hao,majeruhi wengine walioachwa ni pamoja na Nurdin Bakari na Thomas Ulimwengu.

Kwa mantiki hiyo wachezaji watakaopeperusha bendera ya Tanzania katika mchezo huo wa mchujo wa kombe la Dunia utakaopigwa kesho ni pamoja na nahodha Juma Kaseja, nahodha msaidizi Aggrey Morris, Mwadini Ally, Deogratius Munishi, Amir Maftah, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Waziri Salum, Shomari Kapombe na Juma Nyoso. 
Wengine ni Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar, Shabani Nditi, Edward Christopher, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Mbwana Samata, Ramadhan Singano, Simon Msuva na John Bocco.


Comments