TRENI YAPOTEZA UHAI WA MSHINDI TOKELEZEIYER INTER-SCHOOL CONCERT


 Marehemu Jackson Thobias enzi za uhai wake
Na.Mwandishi wetu.

Kijana mdogo wa miaka 17, Jackson Thobias aliyekuwa akisoma kidato cha nne ESACS Academy, amefariki kwa kugongwa na treni maeneo ya kwao kipawa, aligongwa akiwa anasikiliza music kwa headphones huku akichati katika simu yake wakati akitembea kwenye reli.

Pamoja na mlio mkubwa wa treni, na juhudi za watu kumpigia kelele kuwa kuna treni inakuja nyuma yake, Jackson hakusikia.

Marehemu Jackson ndio aliye shinda kwenye Tokelezeiyer Inter-School concert iliyoandaliwa na group  ya Friends 4 Friends tarehe 12 may 2012, pia alishinda dougie competition  wakati 5select Event ya EATV ilipotembelea ESACS wiki mbili zilizopita.

Alikuwa ni kijana mwenye kipaji na ndoto nyingi katika umri mdogo wa miaka 17, Mungu aipumzishe roho ya marehemu Jackson Thobias kwa amani, Amen.

--