TANZIA
MAREHEMU MZEE ANDREW ALLEN SINAMTWA (74)

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya DISEJI ambayo ni kampuni tanzu ya TRETEM, inayomiliki vyuo vya Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ) na Dar es salaam (DSJ), Mzee Andrew Allen Sinamtwa amefariki dunia Juni 18, 2012. 
Taarifa iliyotolea na Mtoto wa Marehemu, Richard Sinamtwa, ambaye ni Mkurugenzi wa Sheria na Uhusino wa Kampuni ya Tumbaku Morogoro, (TLTC), mazishi ya marehemu  yatafanyika Jumatano 20/6/2012, kijijini kwake Mangalali, wilaya ya Iringa Vijijini,Mkoani Iringa. Msiba wa Marehemu upo nyumbani kwake eneo la Nane Nane, mjini Morogoro. 
Marehemu alizaliwa tarehe 2 Februari, 1938 huko Kalenga, Iringa. Kati ya mwaka 1950 na 1953 alipata elimu ya sekondari Malangali, Iringa. Mwaka 1954 hadi mwaka 1956 alipata mafunzo ya ualimu katika Chuo cha Ualimu Butimba, Mwanza. 
Mwaka 1957 alifundisha shule ya kati (District School) Tinde huko Shinyanga. Kisha alijiunga na shirika la Reli la Afrika Mashariki mwaka 1958 ambapo alifanya kazi nalo hadi Mwaka 1993 alipostaafu kazi na kuanza kujishughulisha na vyuo vya uandishi wa habari katika mtandao wa TRETEM. 
Marehemu amekuwa alisumbuliwa na Saratani ya Ini tangu mwaka jana, ambapo aliwahi kupelekwa nchini India kwa matibabu na aliporejea alilazwa katika hospitali ya Hindu Mandal Dar es Salaam hadi umauti ulipompata. 
Marehemu ameacha mke, watoto 9 na wajukuu kadhaa.