STARS YALALA 2-0 DHIDI YA IVORY COAST

MABAO ya Solomon Kalou dakika ya 18 na Didier Drogba dakika ya 80, usiku huu yameizamisha timu ya soka ya taifa ya Tanzania 2-0 katika mchezo wa kwanza wa Kundi C kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.
Pamoja na Stars kufungwa kwenye mechi hiyo Uwanja wa Félix Houphouët-Boigny mjini Abidjan, lakini ilicheza soka safi ya kutia matumaini.
Katika mchezo huo, Stars ilimpoteza beki wake Aggrey Morris dakika ya 70 baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano, baada ya awali kuonyeshwa kadi ya njano dakika ya 12.
Huo ulikuwa mchezo wa pili kwa kocha Mdenmark Kim Poulsen tangu arithi mikoba ya Jan Poulsen Mdenmark mwenzake.
Vikosi vilikuwa; Ivory Coast: B. Barry, K. Touré, S. Tiéné, I. Lolo, E. Eboué, C. Tioté/Ya Konan, K. Coulibaly, J. Gosso, D. Drogba, S. Kalou/M. Gardel na Y. Gervinho/A. Keita.

Tanzania; J. Kaseja, A. Morris, K. Yondani, A. Maftah, S. Kapombe, M. Ngassa, S. Nditi,

M. Kazimoto, S. Abubakar, M. Samatta na F. Domayo.

Comments