SIMBA YAACHANA NA DANNY MRWANDA, NYOSO ALETA POZI


MABINGWA  wa  ligi kuu soka Tanzania Bara, Simba wamefuta mpango wa kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wao Dan Mrwanda (Pichani) anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya DT Long An ya Vietnam, imfahamika.
 Mmoja ya viongozi wa Simba alisema jana kwamba, wameamua kuachana na Mrwanda kufuatia masharti aliyewapa, sambamba na dau la shilingi Mil.12 alilolitaka ili kuweza kumwaga wino. 
“Tumeamua kuachana na Mrwanda kwani pamoja na kutaka dau la mil.12, pia ametaka mkataba atakaousaini umruhusu kwenda nje iwapo atapata timu ya kuichezea, kitu hicho hatukubaliani nacho kwani ni sawa na kutupa fedha,”alisema kiongozi huyo.
Kama hiyo haitoshi, kiongozi huyo aliongeza kuwa bado wapo katika majadiliano juu ya kuongeza mkataba wa beki wao Juma Nyoso ambaye ameonekana kuvimba kichwa baada ya kuondoka kwa Kelvin Yondan, hivyo kutaka aongezewe dau.

Katika hatua nyingine, baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wakiwemo nyota wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao wa  Ligi  na michuano ya kimataifa wameanza mazoezi.
mwisho