SIMBA SC KWENDA MWANZA IJUMAA


KIKOSI cha mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba Sc kinatarajiwa kwenda jijini Mwanza ijumaa hii  kwa ajili ya kupeleka ubingwa wa ligi hiyo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema kwamba kikosi hicho  jumamosi kitacheza jijini Mwanza  na timu itakayotangazwa baadaye kabla ya jumapili kukwaana na Toto Africans katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. 
Baadhi ya wachezaji wa Simba walianza mazoezi ya uwanjani jana kwenye viwanja vya TCC Chang’ombe kwa ajili ya kujiandaa michuno ya Kagame inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi jijini Dar es Salaam juni 14.