SIMBA KUPELEKA KOMBE KANDA YA ZIWA


MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Simba wanatarajiwa wanatarajiwa kufanya ziara maalumu  ya kupeleka ubingwa wao wa ligi kuu soka Tanzania Bara 2011/2012 kwa mashabiki wao wa  mikoani ambapo wataanzia Kanda ya Ziwa.
Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage amesema kwamba kikosi cha timu hiyo kinatarajiwa kuondoka jijini Dar es Salaam julai 15 ambapo Julai 16 watacheza na Toto African katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, kabla ya Julai 17 kukwaana na moja ya timu kutoka nje ya nchi kwenye dimba la CCM Kirumba, jijijini Mwanza.
Rage alisema baada ya ziara ya Kanda ya Ziwa, itafuata ile ya Kanda ya Kusini ambayo itahusisha mikoa ya Lindi na Mtwara.
Aidha, Rage aliongeza kuwa uongozi unaendelea na usajili wake wa wachezaji ambao watakitumikia kikosi hicho katika msimu ujao wa ligi na michuano ya kimataifa.

Comments