SHIWATA LAANDAA TAMASHA LA KUCHANGIA UJENZI WA NYUMBA ZA WANACHAMA WAKE

Na Mwandishi Wetu
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)imeandaa Tamasha la Watani wa Jadi Juni 23, 2012 katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa lengo la kukusanya fedha ili kujenga nyumba za wasanii, waandishi wa habari na wanamichezo katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga.

Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa katika tamasha hilo kutakuwa mchezo wa kikapu (Basketball) utakaochezwa na ngongoti ambao ni wapinzani wa jadi katika mchezo huo.

Taalib alisema msanii wa filamu nchini Lumole Matevolwa (Big) atapambana katika mchezo wa mieleka na mpinzani wake wa siku nyingi mwanamuziki machachari wa bendi ya dansi ya Msondo, Roman Mng'ande (Romario).

Alisema kunatakuwa na vikundi maarufu vya ushangiliaji vya Mpira Pesa (Simba)na Yanga Bomba (Yanga) ambao mbali ya kushiriki kushangilia timu zao katika mapambano mbalimbali yatakayowapambanisha watani hao wa jadi wao pia watacheza.

Alisema Kikundi cha Mpira Pesa wataoneshana ufundi katika soka na wapinzani wao Yanga Bomba na kutakuwa na mpambano wa wazee wa Sunderland (sasa Simba) kuvutana kamba na wazee Yanga Africa piamashabiki wa Simba na Yanga watavutana kamba,

Nao wazee wa Simba na Yanga watavutana kamba pia kutakuwa na pambano kati ya wachezaji maarufu waliowahi kuchezea Simba na yanga.

Taalib alisema kutakuwa na burudani ya ngoma za asili pamoja na bendi ya muziki wa dansi ya Msondo na kuwataka wanachama wa SHIWATA katika mkutano wa wanachama wote Jumamosi Juni 16 makao Makuu yao Splendid Ilala kuanzia saa 3 asubuhi kukamilisha tamasha hilo
.

Comments

Post a Comment