MUZAMIL KATUNZI, YONO KEVELA WAJITOSA YANGA


                                      Yono Kevela

WADAU maarufu wa michezo nchini, Muzamil Katunzi na Yono Kevela ni miongoni mwa wanachama wa klabu ya Yanga ambao wamejitosa kuwania nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Julai 17.

Katibu wa kamati ya uchaguzi ya Yanga Francis Kaswahili ameiambia mamapipiro blog kwamba mpaka sasa idadi ya wagombea imefikia 18 ambapo zoezi la kuchukua na kurudisha fomu litamalizika kesho saa 10 jioni.

Comments