MILOVAN AKARIBIA 'KUJIFUNGA' TENA SIMBA SC


Kocha mkuu wa Simba Milovan Cirkovic ataanza kukinoa kikosi chake kesho kwenye viwanja vya TCC Chang'ombe.
Aidha, kocha huyo anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa kukinoa kikosi hicho wakati wowote.
 Milovan ambaye alikuwa kwao Serbia kwa mapumziko, aliwasili usiku wa kuamkia leo.
Wachezaji wa Simba walianza kujinoa mapema mwezi huu kwa kufanya mazoezi ya kujenga mwili ‘Gym’ kabla ya kuhamia uwanjani hivi karibuni ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao ya michuano ya kombe la kagame linalotarajiwa kuanza juni 14 jijini Dar es Salaam.
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga alisema kwamba Milovan ataanza kazi yake hiyo ambayo ilikuwa chini ya kocha msaidizi Richard Amatre na kocha wa timu ya vijana Amri Saidi. 
Alisema kikosi cha Simba kilichokuwa kanda ya Ziwa kwa ziara maalum kilitarajiwa kuwasili usiku wa leo ambapo wachezaji wachezaji wake wataanza mazoezi jioni ya kesho.
 Kamwaga alioongeza kuwa mazoezi hayo pia yatahusisha nyota wake waadamizi wanaokipiga katika timu ya Taifa wakiwemo Juma Kaseja, Haruna Moshi ‘Boban’, Mwinyi Kazimoto na Amir Maftah ambao walipewa mapumziko ya wiki moja.