MATOLA KOCHA MPYA AFRICAN LYON

NAHODHA wa zamani wa Simba Suleiman Abdallah Matola (pichani)amepewa jukumu ya kuinoa klabu ya African Lyon inayoshiriki ligi kuu soka Tanzania Bara, imefahamika.
Matola ambaye kabla ya kukabidjhiwa jukumu hilo alikuwa kocha wa timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Simba Sc, amesema anashukuru kwa kupewa jukumu hilo ambapo atatumia uwezo wake wote kuhakikisha anaipatia mafanikio timu hiyo.
Amesema kikubwa kinachohitajika ni ushirikiano baina yake, viongozi na wachezaji na ndipo malengo yatatimia.