KUELEKEA UCHAGUZI WA VIONGOZI YANGA:TFF YAWAHADHARISHA WANACHAMA


WAKATI zoezi la uchukuaji fomu za kuwania uongozi katika klabu ya Yanga likianza leo, kamati ya  uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limewataka wanachama wake kufuata kanuni za uchaguzi zilizowekwa na shirikisho hilo. 
Hatua hiyo inafuatia baadhi ya wanachama wa klabu ya Yanga kukiuka kanuni hizo kwa kutoa taarifa potofu kuhusiana na uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi za zilizowazi utakaofanyika Julai 15mwaka huu. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF Deogratius Lyatto alisema jana kwamba uchaguzi huo ni kwa ajili ya kuziba nafasi za viongozi ili kutimiza akidi na si kwa ajili ya kuchagua upya viongozi kama inavyoenezwa. 
“Kuna upotoshwaji unafanywa na baadhi ya wanachama kuhusiana na uchaguzi huu, napenda ieleweke kuwa, uchaguzi huo utajaza nafasi za viongozi waliojiuzulu na ile ya mjumbe mmoja aliyefariki dunia, hivyo wanachama wa Yanga wafahamu hilo na kuzingatia,”alisema. 
Mbali na hilo, Mwenyekiti huyoa lisema kwamba viongozi watakaochaguliwa watakaa madarakani kwa muda uliosalia kama katiba inavyoelekeza na kwa mantiki hiyo hiyo viongozi hao watamaliza muda wao wa miaka minne mwaka 2014. 
“TFF inaamini kuwa wajumbe wa kamati ya uchaguzi wa Yanaga wqatatekeleza wajibu na majukumu yao ya kikatiba na kikanuni kuhakikisha kwamba klabu hiyo inajaza nafasi zilizowazi  katika mkutanio mu wa uchaguzi kwa kipindi kilichobaki cha mamlaka ya kamati ya utendaji (ibara ya 29 ya Katiba ya Yanga),”alisema. 
Kwa mujibu wa Katibu wa kamati ya uchaguzi ya Yanga Francis Kaswahili,  zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu litamalizika Juni 6, huku Juni 7 hadi 13 kamati itapitia  majina ya walioomba kugombea na kutangaza majina yao, wakati juni 14 hadi 18 itakuwa ni kipindi cha kupokea pingamizi. 
Aidha, Juni 19 hadi 23 utafanyika usaili na kutangaza matokeo, wakati juni 24 hadi 26 itakuwa ni kipindi cha kukata rufaa, juni 27 hadi julao mosi kamati ya uchaguzi TFF itasikiliza rufaa kama zipo, huku Julai 2 yatatabgazwa majina na kampeni kuanza hadi julai 14. 
Uchaguzi huo unafuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti Lloyd Nchunga  baada ya kushinikizwa na baadhi ya wanachama wakiongozwa na baraza la wazee wa klabu hiyo kutokana na kushindwa kuiletea mafanikio klabu hiyo chini ya uongozi wake. 
Pia nafasi ya Makamu mwenyekiti iliyokuwa inashikiliwa na Davis Mosha ambaye alijitoa miezi michache baada ya kuchaguliwa kutokana na kutoelewana na Nchunga, huku mjumbe Theonest Rutashoborwa akitangulia mbele ya haki.  
Uchaguzi huo pia utajaza nafasi za Wajumbe  walioachia ngazi ambao ni pamoja na Mzee Yusuf, Charles Mgondo na Ally Mayay. 
Kwa sasa Yanga imebaki na wajumbe wanne, Mohammed Bhinda, Sarah Ramadhan, Tito Osoro na Salum Rupia ambao baada ya uchaguzi wataungana na viongozi wapya na  kuteua wajumbe wengine watatu kwa mujibu wa katiba, hiyo inatokana na wajumbe hao wa kuteuliwa Seif Ahmed, Mbaraka Igangula na Pascal Kihanga kujiuzulu.
.

Comments