KIGOGO WIZARA YA MADINI,MKUU WA WILAYA WAINGIA MITINI YANGA

KATIBU Mkuu wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Handen Muhingo Rweyemamu ambao walijitokeza kuwania uongozi katika klabu ya Yanga wameshindwa kurejeshwa fomu hivyo kujiengua wenyewe katika uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Julai 15.
Katibu Mkuu wa kamati ya uchaguzi Francis Kaswahili amesema leo kwamba  mpoka zoezi hilo kugungwa saa 10.00 jioni Maswi na Muhingo ambao walioomba kugombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji hawakurejesha fomu.
Alisema mbali na hao, wengine walioshindwa kurejesha fomu ni Muzamil Katunzi ambaye alikuwa nagopmbea nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji poamoja na Isack Chanji aliyekuwa anagombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti.

Comments