FIRST EVELEN STARS NA IVORY COAST HII HAPA

Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa, Kilimanjaro Taifa Stars wakiwa kwenye mazoezi ya mwisho kujiandaa na mechi yao ya mchujo ya kusaka tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coastá leo katika Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan, Ivory Coast.
Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa, Kilimanjaro Taifa Stars wakiwa kwenye mazoezi ya mwisho kujiandaa na mechi yao ya mchujo ya kusaka tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coastá leo katika Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan, Ivory Coast.









Kocha wa Makipa wa Kilimanjaro Taifa Stars, Juma Pondamali akiwanoa makipa wa timu hiyo ikiwa ni hatua ya mwiso kabla ya kuvaana na Ivory Coast kesho kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan, Ivory Coast
Mshambuliaji mahiri wa Kilimanjaro Taifa Stars, Mbwana Samatta akiweka saini kwenye madaftari ya vijana wa Ivory Coast mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya kujiandaa na mechi yao ya mchujo ya kusaka tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast katika Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan, Ivory Coast. Samatta amekuwa kivutio kikubwa kwa vijana wengi wa Ivory Coast.

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya taifa, ya Tanzania, Kim Poulsen amesema atatumia mfumo wa 4-4-2 na ametaja kikosi chake cha leo dhidi ya Ivory Coast kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny mjini Abidjan katika mechi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014.
Amefanya mabadiliko katika nafasi mbili kwenye kikosi ambacho Mei 26 mwaka huu kilicheza mechi ya kujipima nguvu na Malawi (The Flames) iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaamna kumalizika kwa suluhu.
Amir Maftah atacheza beki wa kushoto badala ya Waziri Salum wakati Mrisho Ngasa atakuwa mmoja kati ya washambuliaji wa mwisho. Ngasa atacheza nafasi ya Haruna Moshi ambaye hayuko na Stars hapa baada ya kuumia mazoezini siku moja kabla ya safari.
Kikosi kamili cha Taifa Stars ambayo itatumia mfumo wa 4-4-2 ni kima ifuatavyo;
Kim amesema kikosi chake kimejiandaa vizuri kwa ajili ya mechi hiyo, na kilichobaki ni kwa wachezaji kudhibitisha maandalizi hayo kwenye dakika 90 za mchezo huo utakaoanza saa 11 kamili jioni (nyumbani itakuwa saa 2 kamili usiku).
Mechi hiyo itaoneshwa moja kwa moja (live) kupitia televisheni ya RTI ambapo itaonekana katika nchi 58 duniani.
Jana Stars ilifanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja ambao watautumia katika mechi ya leo na baada ya mechi hiyo, mshambuliaji Mbwana Samatta wa Tout Puissant Mazembe ya DRC alifuatwa na mashabiki walioomba kuwatilia sanini.
Mashabiki hao walivutiwa na soka ya Samatta na tayari mpachika mabao huyo ghali zaidi kuwahi kuuzwa kutoka Tanzanani akitokea Simba SC msimu uliopita amekuwa gumzo mno nchini hapa.
Kwa ujumla mazoezi ya jana ya Stars yamewatia homa kiasi fulani wenyeji, kutokana viwango vilivyoonyeshwa na wachezaji na wanaamini leo wanakutana na timu ya ushindani.    

KIKOSI KAMILI; Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Amir Maftah, Aggrey Morris na Kevin Yondani, Shabani Nditi, Salum Abubakari, Frank Domayo na Mwinyi Kazimoto, Mbwana Samata na Mrisho Ngasa.
BENCHI; Mwadini Ali, Waziri Salum, Juma Nyoso, Erasto Nyoni, John Bocco, Simon Msuva, Jonas Mkude, Christopher Edward na Ramadhan Singano

Comments