EXPRESS YAITAKA YANGA KUIRUDISHA AYE

Meneja wa timu ya Express FC, Mahmoud Katerega akizungumza na katibu mkuu wa Yanga Mwesigwa Selestine, makao makuu ya klabu

Mabingwa wa soka nchini Uganda Express F.C wamesema wapo tayari kuwa na mahusiano ya karibu kati yake na Mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati Young Africans Sports Club (YANGA) kama ilivyokuwa katika miaka ya sabini. 
Akizungumza na Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga Mwesigwa Selestine, Meneja wa timu ya Express Mahamod Katerega amesema iwapo timu hizo zikiimarisha mahusiano ya karibu kama zamani zitapata maendeleo ya kutosha katika sekta ya uchumi pamoja na mchezo wenyewe wa mpira wa miguu.
Katerega amesema katika miaka hiyo ya sabini timu tatu za Afrika Mashariki ikiwemo Abaluya FC ya Kenya,Yanga ya Tanzania na Express ya Uganda zote kwa pamoja zilikuwa na umoja uliojulikana kama (AYE) ambapo timu hizo zilikuwa zikishirikiana na kucheza michuano maalum kila mwaka.
Meneja huyo wa Express amesema wakati umefika kwa timu zilizopo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kuwa na mahusiano ya karibu ili kuweza kupata maendeleo ya haraka kama wanavyofanya timu mbalimbali za Ulaya na nchi za ASIA
Timu ya Yanga na Express zinatarajia kushuka dimbani jioni ya leo katika uwanja wa taifa jijini Dar Salaam ikiwa ni maandalizi kwa timu hizo katika michuano ya Kombe la Kagame na maandalizi ya ya lgi kuu.
CHANZO:www.youngafricans.co.tz