ALI MAYAY AENGULIWA UCHAGUZI YANGA SC

NYOTA wa zamani wa Yanga aliyeemba kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti katika klabu hiyo, ameenguliwa katika kinyang'anyoro.
Kamati ya uchaguzi ya Yanga chini ya Mwenyekiti wake Jaji Mstaafu John Mkwawa iliketi jana kupitia pingamizi zilizowekwa ambapo Mayay alikuwa mmoja ya wagombea waliopigwa.
Hata hivyo Mayay ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya Utendaji ya uongozi ulijiuzulu chini ya mwenyekiti Lloyd Nchunga, alishindwa kufika katika kikao hicho cha kujadili mapingamizi, hivyo kamati kumuengeua.
Hata hivyo, Mayay amesema hakuwa anafahamu kuwa jana alitakiuwa kuhudhuria kikao hicho hivyo amekusudia kukata rufaa.
Mbali na Mayay wagombea wengine waliokuwa wamewekewa pingamizi ni pamoja na Yussuf Manji anayegombea nafasi Mwenyekiti na Clement Sanga anayewania Makamu Mwenyekiti katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika JUlai 15 jijini Dar es Salaam.