YANGA WAWASILI MILINGOTINI KUSAKA DAWA YA SIMBA

KIKOSI cha timu ya Yanga mchana huu kimewasili mjini Bagamoyo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake wa mwisho wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Simba utakaopigwa jumamosi kwenye dimba la taifa.
Taarifa ambazo mamapipiro blog imezinasa zinaeleza kwamba Yanga imewasili mjini humo na kufikia katika hoteli ya Kiromo View.
Wakati Yanga wakijichimbia huko, mahasimu wao Simba wapo Zanzibar tangu jana ambapo timu inaendelea na mazoezi yake katika uwanja wa Fuoni huku ikiwa imepiga kambi eneo la Mbweni.

Comments