WASANII KUTOKA MFUMO WA ANALOGIA KWENDA DIGITAL

Msimamizi wa vipindi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Mwanga Kirahi akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada iliyohusu Teknolojia ya kisasa (Digital) Katika Utengenezaji Filamu kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA wiki hii.Kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Matukio BASATA, Malimi Mashili.
Mkongwe wa Muziki wa dansi Mzee Kassim Mapili akionesha manjonjo yake baada ya kufurahishwa na mada kuhusu Mfumo Digital iliyowasilishwa kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii.
Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Mawasiliano ya Umma Ngalimecha Ngahyoma akichangia mada hiyo kwenye Jukwaa la Sanaa. Alishauri Wasanii kujipanga katika kuukabili mfumo wa Digital.
Sehemuya Wadau wa Jukwaa la Sanaa waliohudhuria mjadala huo wakifuatilia kwa makini. Na Mwandishi Wetu Wasanii nchini wameshauriwakujipanga katika kutumia fursa na changamoto mbalimbali zitakazojitokeza wakatiUlimwengu ukijiandaa kuingia kwenye mfumo wa digital kutoka ule wa nalogia ifikapo mwaka 2014. Ushauri huo umetolewa wikihii na Msimazi wa Vipindi vya televisheni wa Shirika la Utangazaji la Taifa(TBC) Mwanga Kirahi wakati akiwasilisha mada iliyohusu Teknolojia ya kisasaKatika Utengenezaji Filamu kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki makaomakuu ya BASATA Ilala Sharif Shamba. Alisema kuwa kuhama kutokamfumo wa analogia kwenda digitali kutazalisha fursa mbalimbali za kuendelezaSanaa nchini lakini pia ni mwanzo wa kuibuka kwa changamto nyingi ambazo kamawasanii hawatakuwa makini basi wanaweza kupotea na kushindwa kushindanaipasavyo. “Mfumo wa digitali utaletaushindani katika kuandaa programu za televisheni, utazalisha fursa kwa kazi zawasaniii wetu kuonekana ulimwengu mzima lakini unaweza kuwa mwanzo wa kufa kwaubunifu kama wasanii watategemea vifaa vya kisasa tu pasipo kuingiza ubunifubinafsi” alisisitiza. Katika hili aliwashauriwasanii kutengeneza kazi zenye ubora na zisizo za kunakiri kutoka kwa wengine lakinipia zenye ubunifu binafsi pasipo kutegemea vifaa hivi vya kisasa pekee kwanikinyume chake ni kukataliwa kwa kazi zao na hatimaye kupwaya. “Digital maana yake ni kaziza Wasanii wetu kuonekana Ulimwengu mzima, sasa kama zitakuwa za kunakirikutoka kwa wengine na kutegemea vifaa hivi vya kisasa tu pasipo ubunifu binafsihatutafanikiwa. Haya pekee yanazifanya kazi zetu zisivume muda mrefu kwanizinakuwa si original (halisi)i” alizidi kusisitiza. Aliongeza kuwa, wasaniihawana budi kubadilika sasa na kuacha tabia ya wao kufanya kila kitu kikuanzia umeneja, utunzi, uongozaji (directing), uzalishaji (producing) nakadhalika kwani kwa kufanya hivyo kunazifanya kazi zao kuwa na radha moja pekeeambayo haiwezi kudumu muda mrefu. Wadau wengi waliofikakupata elimu hiyo kupitia programu ya Jukwaa la Sanaa waliiomba Mamlaka yaMawasiliano nchini (TCRA) kupanga kukutana na wasanii ili kuwapa elimu juu yamchakato wa kuhama kutoka mfumo wa analogia kwenda digitali.

Comments