WACHEZAJI WA SIMBA KUTEMBEZWA JIJI ZIMA J'2

KLABU ya soka ya Simba imewaaalika wadau wote na wanachama wa timu hiyo kuhudhuria sherehe maalum za ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara zitakazofanyika jumapili ya Mei 27 kwenye ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange 'Kaburu' ameiambia mamapipiro blog kwamba, siku hiyo kutaanzwa kusomwa dua makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Msimbazi jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza msafara wa wachezaji kupitia barabara ya Morogoro hadi Ubungo ambapo watasimama katika matawi ya Mpira Pesa na Ubungo Terminal.
"Wakitoka ububgo watapita Mandela road mpaka buguruni ambapo watasimama kidogo na kisha kupitia barabara ya Uhuru, Karume, Uwanja wa Taifa hadi Dar Live, ambapo shughuli zitaanza saa kumi jioni,"alisenma.
Kaburu aliongeza kuwa sherehe hizo zitapambwa na burudani toka Mashauzi Classic, Msondo Ngoma na Yong D huku kiingilio kikiwa nish.5,000 na 20,000 kwa viti maalum.

Comments