TFF YAWAONYA WAAMUZI, WASIMAMIZI WA VITUO MECHI ZA MWISHO


SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limesema litahakikisha linadhibiti hujuma ya aina yoyote katika michezo ya mwisho ya ligi kuu soka Tanzania bara itakayorindima jumapili ya keshokutwa.
Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah amesema leo kwamba katika kusimamia hilo wamewaonya makamishina na makamisaa wote kuhusu muda wa kuanza pambano.
Alisema kuwa wamewaandikia barua wasimamizi wote wa vituo pamoja na makamisaa kuhakikisha mechi zote za Ligi kuu zinaanza saa 10:00 alasiri.
Aiongeza kuwa timu zote 14 zinazoshiriki Ligi kuu zitashuka dimbani katika viwanja saba tofauti na kwa kuwa mechi hizo ndizo zinazotarajiwa kumtoa bingwa wa msimu huu, mshindi wa pili na timu ya tatu kushuka daraja, inabidi muda wa kuanza na kumaliza mchezo ulingane.
“Katika kuhakikisha kuwa hakuna upangaji matokeo unaofanyika tumewandikia barua wasimamizi wa vituo na makamisaa wote kuhakikisha mechi zote za Ligi kuu zitakazochezwa Jumapili ‘kesho’ zinaanza saa 10:00 yeyote atakayekiuka atachukuliwa hatua kali za kinidhamu,” alisema Osiah.

Comments