TFF KUJADILI HATMA YA UONGOZI WA YANGA



Kwa vile wajumbe kadhaa wa Kamati ya Utendaji ya Yanga akiwemo Mwenyekiti wa kamati hiyo Lloyd Nchunga wamejiuzulu, Kamati ya Uchaguzi ya Yanga imeliandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikitaka mwongozo juu ya hilo. 
Kwa kuzingatia hilo, TFF imepeleka suala hilo kwa kamati yake ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ili itoe maoni yake kisheria ya nini kinafanyike kuhakikisha Yanga inaendelea na shughuli zake kama kawaida. 
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa inatarajia kukutana leo jioni kushughulikia suala hilo na baadaye Kamati ya Uchaguzi ya Yanga pamoja na Kamati ya Uchaguzi ya TFF zitapewa maelekezo ya kufanya kwa kuzingatia taratibu zilizopo. 
 

Comments