TASWA, TPBO WAMLILIA MAFISANGO

TASWA imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha kiungo wa timu ya Simba ya Dar es Salaam na mchezaji wa timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi), Patrick Mutesa Mafisango kilichotokea alfajiri ya Alhamisi kwa ajali ya gari jijini Dar es Salaam.
TASWA inatoa pole kwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage, wachezaji wa timu hiyo, mashabiki na Watanzania kwa ujumla kutokana na msiba huo mkubwa kwa familia ya mpira wa miguu.
Tunaamini waandishi wa habari za michezo wameguswa kwa kiasi kikubwa na msiba huo, kwani wakati wa uhai wake marehemu alikuwa na ushirikiano mkubwa na wanahabari na hakuwa mtu mwenye maringo, kiasi cha kushindwa kutoa ushirikiano kwa wenzake.
Tunasema kifo chake ni pigo si kwa Simba na familia yake tu, bali hata kwa timu ya Taifa ya Rwanda na Wanyarwanda wote, ambao pia tunawapa pole kwa msiba huo.
Tunawapa pole wanamichezo wote na kuwaomba wawe na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu, huku wakiamini waandishi wa habari za michezo tupo nao pamoja katika majonzi hayo na kumuomba Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peoni. Amina.

 Kifo cha Mzee Limonga
Tunapenda kuwajulisha waandishi wa habari za michezo wote pamoja na wadau wengine kuwa mtangazaji wa habari za michezo wa Redio Uhuru, Limonga Justine, amefiwa na baba yake mzazi jana Alhamisi asubuhi kwenye hospitali ya Temeke, Dar es Salaam .

Msiba upo Mbagala kwa Mangaya, Dar es Salaam na maziko yanatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi. Naomba tuungane naye mwenzetu katika kipindi hiki kigumu kwake na tumfariji kwa kadri tuwezavyo kwa kuondokewa na mzazi wake. Nambari yake ya simu ni 0713-604578.


Nawasilisha.

Amir Mhando

Katibu Mkuu TASWA

18/05/2012.

0713-415346

KWA MASIKITIKO MAKUBWA SANA NAPENDA KUTOWA SALAMU ZANGU ZA RAMBIRAMBI NA KUWAPA POLE VIONGOZI WOTE ,WANACHAMA WOTE NA WAPENZI WOTE WA SIMBA SPORTS CLUB YA JIJINI DSM ,KWA MSIBA MKUBWA SANA ULIOWAPATA KWA KUONDOKEWA UHAI KWA MCHEZAJI WAO MAARUFU -PATRIC MAFISANGO.
SISI VIONGOZI WA TPBO PAMOJA NA KUWA NI VIONGOZI WA MCHEZO WA NGUMI LKN PIA HUPENDELEA SANA KUHUDHURIA KUANGALIA MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU ,KWANI NI MOJA A BURUDANI TUIPENDAYO PIA,.
HIVYO BASI TUNATAMBUWA SANA NA KUHESHIMU MCHANGO MKUBWA SANA AMBAO MAREHEMU PATRIC MMAFISANGO ALIUTOWA KWA TIMU YA SIMBA PAMOJA NA WATANZANIA KWA UJUMLA HASA VIJANA WADOGO WAPENDAO KUCHEZA MPIRA WA MIGUU-MAFISANGO ALIKUWA NI KIGEZO KWAO.
MMI BINAFSI WAKATI NIKIHUDHURIA MICHEZO MBALIAMBALI ILIYOKUWA IKCHEZWA NA KLABU YA SIMBA NILISHUHUDIA MCHANGO MKUBWA ALIOKUWA AKIJITOLEA UWANJANI NA KUIFANYA SIMBA SPORTS CLUB KUWA MSHINDI ,NA HATIMAYE KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU YA VODA-COM MWAKA HUU..
TPBO INAPENDA KUWAFARIJI WACHEZAJ WOTE WA SIMBA SPORTS CLUB KWA MSIBA HUO ,PAMOJA NA KWAMBA ITAWACHUKUWA MUDA MREFU SANA KUSAHAU KIFO CHA MAFISANGO ,NINAWAOMBEA KWA MUNGU ILI AWAPUNGZIE MAJONZI NA WALIONE HILI NI JAMBO LILILOPANGWA NA YEYE MWENYEZI MUNGU MUUMBA WETU ,PIA WAZIDISHE KUMUOMBEA MUNGU ILI AMSAMEHE MAKOSA YAKE NA AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI -AMEIN
NA NJIA NYINGINE YA KUMUENZI MCHEZAJI MWENZAO NI KUHESHIMU KAZI YAKE YA UWANJANI, NA WAIGE ALIVYOKUWA AKIJTUMA AWAPO UWANJANI, NA NIDHAMU YAKE ALIPOKUWA UWANJANI,. KWA KUTENDA HAYO WATAKUWA WANAMUENZI VYEMA.
BWANA AMETOWA ,NA BWANA AMETWAA- NENO LA BWANA LIHIMIDIWE-
EEH BWANA UMPE RAHA YA MILELE PATRIC MAFISANGO NA MWANGA WA MILELE UMUANGAZIE ,NA ASTAREHE KWA AMANI.AMEEN
YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
RAIS-TPBO

Comments