STARS YAWAFUATA KINA DROGBA BILA BOBAN, CHOLLO




WAKATI kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars' kikiondoka alfajir ya leo kuelekea nchini Ivory Coast, wachezaji nyota wa  klabu ya Simba, beki Said Nassor 'Chollo' na kiungo Haruna Moshi 'Boban' wameondolewa kwenye kikosi hicho.
Wachezaji hao wameondolewa kutokana na kuwa majeruhi hivyo kufanya msafara huo kuwa na wachezaji 21.
Awali nyota wawili wa kikosi hicho Nurdin Bakari wa Yanga na Thomas Ulimwengu anayekipiga klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walipata majeruhi kabla ya hali zao kuimarika.Hata hivyo nyota hao pia wameachwa ili kuendelea kujinoa taratibu na wataungana na wenzao watakaorejea juni 5.
Stars na  Ivory Coast zitamenyana juni 2 katijka mechi ya  mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia itakayopigwa dimba la Felix Houphouet-Boigny jijini Abijan kuanzia saa 11 kamili kwa saa za Ivory Coast.
Mchezo huo utachezeshwa na Mwamuzi atakuwa Slim Jedidi wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Bechir Hassani, wote kutoka Tunisia. Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Sherif Hassan kutoka Misri. Mwamuzi wa akiba ni Youssef Essrayri pia kutoka Tunisia.
Mtathmini wa waamuzi ni Rachid Medjiba kutoka Algeria wakati Kamishna wa pambano hilo atakuwa Saleh Issa Mahamat kutoka Chad.

 Wachezaji waliokwenda Ivory Coast ni pamoja na  Nahodha Juma Kaseja, Nahodha msaidizi Aggrey Morris, Mwadini Ally, Deogratius Munishi, Amir Maftah, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Waziri Salum, Shomari Kapombe, Juma Nyoso, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar, Shabani Nditi, Edward Christopher, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Mbwana Samata, Ramadhan Singano, Simon Msuva na John Bocco.

Comments