SIMBA WAIFUATA SHANDY BILA CHOLLO, NYOSO


WAWAKILISHI wa Tanzania katika kombe  barani Afrika (CAF) Simba inaondoka nchini mchana wa kesho  kwenda Sudan huku ikiwaacha nyota wake kadhaa wakiwemo Juma Nyoso na Ulimboka Mwakingwe, Nassoro Said ‘Chollo’ imefahjamika. 
Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ameiambia mamapipiro blog kwamba  wachezaji hao wameachwa kutokana na sababu mbalimbali, huku wale waliomo katia msafara humo wakiwa na ari kubwa ya mchezo huo.
Alisema kuwea msafara wa watu 25 wakiwemo wachezaji 20 na viongozi watano wataenda huko  tayari kwa mchezo wao wa marudiana na Al Ahli Shandi ya huko utakaopigwa jumapili hii. 
Alisema msafara huo utakaokuwa chini mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Hussein Mwamba utaondoka kwa ndege ya Shirika la Kenya (KQ), ambapo wachezaji wote watakaokwenda huko wapo katika hali nzuri. 
Aliongeza kuwa uongozi unamatarajio makubwa ya timu hiyo kusonga mbele kutokana na matayarisho waliyoyafanya huku wakichagizwa zaidi na kutwaa ybingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara iliyomalizika jumapili iliyopita. 
Hata hivyo Kaburu alisema wataenda Sudan wakiwa na tahadhari kubwa kutokana na ukweli kwamba wapinzani wao watafanya kila njia kutokana na uenyeji wao kuhakikisha wanatumia vema uwanja wa nyumbani.
“Kama mnavyojua tuliwafunga Shendi tulivyocheza naop sasa sidhanui kama watabweteka na kutaka kufungwa kirahisi, kwa hali hiyo tumejipanga ipasavy kukabiliana na hali yoyote tutakayokutana nayo huko ili kuweza kushinda,”alisema Kaburu. 
Katika mchezo wa awali uliopigwa nchini wiki iliyopita Simba iliifunga Shendi mabao 3-0 katika mchezo hivyo inahitaji kulinda ushindi wake kwa namna moja ama nyingine ili kusonga mbele.

Comments