SIMBA SC YACHIMBA BONGE LA MKWARA

Simba SC imesikitishwa na taarifa zisizo za ukweli kumhusu Emmanuel Okwi kujiunga na timu yoyote ya hapa nchini. Mchezaji mwenyewe ameeleza pia kushangazwa kwake na Uongozi wa Simba unawaomba wapenzi na wanachama wake kupuuzia taarifa zozote kuhusiana na Okwi au mchezaji mwingine yeyote wa Simba katika kipindi hiki. Hata hivyo, uongozi wa Simba unasisitiza kwamba Okwi ana mkataba na timu yake na inamhitaji kumtumia msimu huu na mingine inayokuja. Kama kuna taarifa zozote za usajili kumhusu Okwi au mchezaji yeyote wa Simba, uongozi utakuwa wa kwanza kuwapa taarifa wapenzi na wanachama wake. Imetolewa na Ezekiel Kamwaga Msemaji Simba SC

Comments