SIMBA KUREJEA KESHO, RAGE AOMBA MAPOKEZI MAKUBWA

WALIOKUWA wawakilishi wa Tanzania katika kombe la Shiriklisho baranmi Afrika (CAF) timu ya soka ya Simba wanarejea nchini kesho wakitokea Sudan walipokwenda kurudiana na Al Ahli Shendi ya huko. Hata hivyo Simba ilitolewa katika michuano hiyo baada ya baada ya kutolewa kwa penalti 9-8 na Al Ahly Shandy ya Sudan kufuatia sare ya jumla ya tatu. Mwenyekiti wa Simba Al hajj Ismail Aden Rage alisema kwamba matokeo hayo ni sehemu ya mchezo hivyo hakuna haja ya kutafuta mchawi kwani vijana wake walicheza kadiri walivyoweza lakini bahati haikuwa yao. Aidha, Rage amewaomba wadau na mashab iki wa Simba kujitokeza uwanja wa ndege kesho kwa ajili ya kuipokea timu hiyo ambayo pamoja na kufungwa huko ilifanya kazi kubwa.

Comments