SIMBA KUANDAA PATI LA KUJIPONGEZA KWA UBINGWA WA VPL

UONGOZI wa Simba SC unatoa salamu za shukrani na pongezi kwa wapenzi na wanachama wake wote kufuatia mafanikio ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Yanga. Uongozi unaomba wanachama wa Simba waendelee kuipa timu yao sapoti na kuendeleza mshikamano uliopo sasa. Mara baada ya timu kurejea salama kutoka Sudan, wanachama watatangaziwa namna shughuli ya kushangilia ubingwa itakavyokuwa

Comments