SEMINA UA UZINDUZI WA KAMPENI YA 100% TZ FLAVA KWA WAANDISHI WA HABARI


 Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager George Kavishe akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari wakati wa semina kuhusiana na kampeni ya 100% Tz Flava. 
Mamapipiro na wadau wengine
 Mamapipiro na wadau wengine

Wadau kutoka kushoto Asha Kigundula (Jambo Leo), Somoe Ng'itu (Nipashe), Vicky Kimaro (Mwananchi) na Zena Chande (Habari Leo)


Na Mwandishi wetu
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager imezindua Kampeni kubwa ijulikanayo kama 100%  TZ Flava yenye kaulimbiu ya ‘Sherekea KilichoChetu’ itakayoendeshwa kwa miezi sita mfulululizo.
Kampeni hiyo ya aina yake inayolenga kuwahamasisha watanzaniakujivunia mambo mbalimbali ya Kitanzania kamavile muziki, lugha na michezo, ilizinduliwa katika Ukumbi wa Nyumbani Lounge.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alizindua penikhiyo akisema kwamba itaendeelea kwa miezi sita kuanzia sasa ikiwa ni mwendelezowa kampeni ya Kili Jivunie uTanzania iliyofanyika mwaka jana kuadhimisha miaka50 ya Uhuru.
Alisema shughuli ya kwanza ilikuwa kuzindua alama ya kampeni hiyo,100% tz Flava- tusherehekee kilicho chetu na nyingine zitafuatia ndani ya miezisita ambapo kampeni hiyo itawafikia watanzania nchi nzima.
“Kampeni hii imeandaliwa kumpa mteja raha, lakini lazima iache ujumbe,ambao ni Sherekea kilicho chetu,”alisema Kavishe. 
Kipa wa Yanga, Shaaban Kado na winga wa Simba Salum Machaku walipambavyema onyesho hilo la uzinduzi ambapo walishiriki kwa pamoja na  pamoja na wasanii wa kundi la THT na waigizajinyota wa filamu Tanzania, Aunt Ezekiel na Jacob Steven ‘JB’, nyota wa muziki waHip hop, Joseph Haule ‘Preofesa Jay’ na mwimbaji wa bendi ya African Stars‘Twanga Pepeta’, Janet Isinike ‘Janet Jackson’ na kushangiliwa kwa nguvu nawaalikwa kwenye sherehe hiyo.
Kwa mujibu wa Kavishe kampeni hiyo imetumia picha za Simba na Yanga,klabu ambazo zinadhaminiwa na bia hiyo. 
katika kampeni hiyo pia wametumia lugha za mtaani, ambazo Kavishealisema ni fahari ya Tanzaniakwa mfano piga tarumbeta, neno linalowakilisha kunywa bia kwa kutumia chupamoja kwa moja na kula bata, yaani kula raha. 
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na wada mbalimbali ambao walpata burudanimurua iliyoenda sambamba na kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager.
Kabla ya uzinduzi huo, Bia ya Kilimanjaro Premium Lager iliendeshasemina kwa waandishi mbalimbali wa habari za michezo na burudani ilikuwaelimisha kuhusu kampeni hii huku Kavishe akisisitiza kuwa wanahabari niwadau muhimu katika kupeleka ujumbe kwa umma hivi ni muhimu kwao kuelewakampeni hii na malengo yake.

Comments