R.I.P PATRICK MUTESA MAFISANGO

 Wachezaji wa Stars a,mbao pia wanakipiga klabu ya Simba, Amir Maftah wakiongoza wenzao mara baada ya jeneza lililobeba mwili wa mchezaji mwenzao Patrick Mafisango lilipowasili katika viwanja vya TCC Chang,ombe tayari kwa kuagwa.
Marehemu ambaye alikuwa mchezaji wa kimataifa wa Simba anatarajia kuzikwa kwao nchini Congo, alifariki kwa ajali ya gari usiku wa kuamkia alhamis eneo la VETA Changombe.

 Wachezaji wa Stars Juma Nyoso kushoto (Simba) na John Bocco 'Adeboyer' (Azam Fc) wakibeba jeneza la MAfisango.
 Mashabiki
 Nahodha wa Simba Juma Kaseja akifarijiwa na mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Simba, Ibrahim Masoud 'Maestro'.
 Rafiki mkubwa wa Marehemu Mafisango, Haruna Moshi 'Boban' akiwa na uchungu mwingi
 Waziri wa Habari Utamaduni na MIchezo, Dk Fenela Mukangara akitoa neno na pole kwa uongozi wa klabu ya Simba kutokana an kuondokewa na mchezaji wao mahiri Mafisango, kulia ni mwenyekiti wa Simba Al Hajj Ismail Aden Rage
 Mrisho Ngasa, kocha mkuu wa Stars Kim Poulsena na Meneja wa Stars Leopard Taso Mukebe
 Mwenyekiti wa zamani wa Simba Hassan Dalali 'Field Marshal' akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa zamani wa Simba Kassim Dewji
 Mamapipiro na wadau wengine tukiaga mwili wa marehemu Mafisango
 Asha Kigundula mwandishi mwandamizi wa michezo na mdau mkubwa wa Simba akiaga
 Baadhi ya wachezaji wa Simba wakiaga mwili wa mwezao
 Emmanuel Okwi akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa mchezaji mwenzake
 Mdogo wa marehemu, Olilemba Mafisango akilia kwa uchungu wakati akielekea kuaga mwili wa kaka yake, hata hivyo alishindwa kufanya hivyo kutokana na uchungu mkubwa aliokuwa nao
 Jamaaa, marafiki na wadau wa Simba wakiaga mwili wa Mafisango


Mkurugenzi wa ufundi wa timu za vijana za Simba Abdalla Kibaden, akiwa na mashabiki pamoja na baadhi ya wachezaji wa Simba
Wandishi wa habari na wadau wa Simba Mwani Nyangasa na Vicky Kimaro wakiaga
Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga akiga
Askari wa JWTZ akitoa heshima za mwisho kwa mafisango,pia mchezaji wa zamani wa Simba ambaye kwa sasa ni kocha wa vijana wa Simba Seleman Matola naye alihudhuria
Mdau mkubwa wa Simba  Profesa Philemon Sarungi akimfariji Rage

Baadhi ya wachezaji wa Stars

Wadau na mashabiki wa Simba waliojitokeza
Mdau mkubwa wa Simba Azim Dewji kati akiwa na madau mwingine Majaliwa Mbassa kushoto na kocha wa Simba, Milovan Cirkovic
 Gari lililobeba mwili wa marehemu mafisango
 Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic akiaga mwili wa MAfisango, nyuma yake ni mwanachama maarufu wa Simba Hassan Othaman 'Hassanoo'
Wadau waliojitokza

Comments