RAIS JAKAYA KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA MAFISANGO


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Alhaj Ismail Aden Rage kufuatia kifo cha kiungo wao wa kimataifa wa Rwanda mwenye silia ya DRC, Patrick Mutesa Mafisango usiku wa kuamkia jana.Rais Kikwete amesikitishwa na kifo cha Mafisango katika umri mdogo na amewapa pole wana Simba wote.Amesema katika kipindi kifupi cha Mafisango kucheza Tanzania amechangia mafanikio ya soka ya Tanzania kupitia klabu yake, Simba. Mwili wa Mafisango umeagwa jana  kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe na kwenda kuhifadhiwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, tayari kusafirishwa leo kwenda Kinshasa, DRC kwa mazishi.

Comments