RAHWA AFEWORK KUIWAKILISHA ERITREA SHINDANO LA MISS EAST AFRIKA



Warembo watakaoziwakilisha Nchi zao katika mashindano ya Miss East Africa mwaka huu wameanza kutangazwa. 
Mrembo wa kwanza kupatikana ni Miss Rahwa Afework (22) kutoka Nchini Eritrea ambae aliwashinda wenzake waliojitokeza kutaka kuiwakilisha Eritrea katika mashindano hayo. 
Miss Rahwa Afework mwenye urefu wa 1.73m anasomea mambo ya Fashion design Nchini Eritrea
Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika tarehe 07 mwezi September mwaka huu jijini Dar es salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius. 
Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam 

Comments