RACHEL KUAGWA, KUZIKWA KESHO DAR

Rachel kulia akiwa na mtoto Cessa enzi za uhai wake MWILI wa aliyekuwa Mhariri wa Habari za Michezo wa gazeti la Mtanzania, Rachel Mwiligwa unatarajiwa kuagwa kesho Jumatatu Mei 14, 2012 saa nne kamili asubuhi katika Kanisa la Anglikana, Ubungo, ambalo lipo nyuma ya majengo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ubungo jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Msemaji wa familia, Alex Chimila, taratibu za kuaga mwili wa marehemu zitaanza saa 4:00 asubuhi na kumalizika saa 6:00 mchana, tayari kwa msafara wa kwenda kuzika katika Makaburi ya Tegeta A, Goba, jijini Dar es Salaam. Alisema uamuzi wa kuaga mwili kwenye eneo hilo una lengo la kutoa nafasi kwa wadau mbalimbali kupata fursa ya kushiriki kwenye tukio hilo. Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Amir Mhando ametoa wito kwa waandishi wa habari za michezo na wadau wengine wa michezo na burudani kujitokeza kwa wingi asubuhi kwenda kumuaga mpendwa wetu. Rachel alifariki dunia usiku wa kuamkia juzi, kwenye hospitali ya Mwananyamla, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu

Comments