OKWI AZUSHIWA KIFO, FUFA YAKANUSHA

SHIRIKISHO la soka nchini Uganda (FUFA) limekanusha taarifa za uzushi zilizoenea nchini humo kwamba mshambuliaji wa kimataifa wa nchi hiyo anayecheza soka la kulipwa nchini Tanzania katika klabu ya Simba, Emmanuel Okwi alifariki katika ajali ya gari iliyomuhusisha pia mchezaji wa timu hiyo, Patrick Mutesa Mafisango.
Kwa mujibu wa mtandao wa FUFA,taarifa hizo za uzushi zilieleza kuwa Okwi ambaye alikuwa nirafiki wa karibu wa marehemu Mafisango alikuwa katika gari moja wakati wakitoka katika klabu ya usiku ya Maisha jijini Dar es Salaam, pamoja na mchezaji mwingine wa Simba, Mganda Derick Walulya.

Comments