NCHUNGA AFUTA MKUTANO YANGA KESHO

MWENYEKITI wa Yanga Lloyd Nchunga amefuta mkutano wake na wazee wa klabu hiyo aliopupanga kuufanya kesho.
Nchunga ameiambia mamapipiro blog mchana huu kwamba ameaamua kuufuta mkutano huyo kutokana na baadhi ya wanachama kutoa taarifa za kupotosha, hivyo ameawata wanachama kusubiri hadi julai 15 ambapo utafanyika mkutano mkuu wa wanachama.
"Nimefanya hivyo ili wasijepotosha kuwa nimeitisha mkutano kinyume na katiba...kwani mimi sijaitisha mkutano mkuu wa wanachama,"alisema.
Nchunga amesema kwamba sababu nyingine ya kuahirisha mkutano huo inatokana na barua waliyopatiwa na aliyekuwa mfadhili mkuu, Yusuf Manji ambapo jumatatu kamati ya utendaji inatarajiwa kukutana kwa ajili ya kujadili.

Comments