MSONDO NGOMA KUZINDUA UKUMBI MPYA WA EMIRATE ULIPO MASASI

Na Mwandishi Wetu
BENDI Kongwe ya Msondo ngoma ya jijini Dar es salaam inatarajia kufanya uzinduzi wa ukumbi mpya kabisa wa kisasa wa burudani  wa Emirate Hall uliopo Masasi June 2 mwaka huu.
Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' Alisema wamealikwa kwa ajili ya kutoa burudani siku ya ufunguzi wa ukumbi huo ambapo watatoa burudani isiyo na kifani
;unajua sisi ni baba ya Muziki nchini ndio mana wapenzi wengi wanaitaji burudani kutoka kwetu ndio mana tunapopata nafasi ya kwenda mikoani tunakwenda kama hivi tumealikwa kutoa burudani siku hiyo tutatoa burudani ya uwakika;siku hiyo tutapiga vibao vetu vya zamani na vipya kwa sasa alivitaja baadhi ya vibao vitakavyonogesha uzinduzi huo kuwa ni Suluhu wa Shabani Dede, Nadhiri ya Mapenzi wa Juma Katundu na Baba Kibene wa Eddo Sanga hizo ni baadhi ya nyimbo mpya zitakazonogesha siku hiyo vile vile watapiga nyimbo zao za zamani zilizotamba wakati huo  Alisema Super D Kundi hilo litaambatana na
wanamziki wake wote wakiwemo wakongwe katika mziki wa Dansi Nchini
Maalimu Gulumo ' Kamana' Saidi Mabela ' DKT Mabela' na wengine wote
watafanya vitu vyao siku hiyo kwa ajili ya kukonga nyoyo za mashabiki
wao wa Masasi Aliongeza Super D

Comments