DIAMOND KUPAMBA MR& MISS IFM KUPATIKANA KESHO CINE CLUB

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Nasib Abdul ‘Diamond’ kesho anatarajiwa kupamba shindano la kumsaka Miss Mr & Miss IFM linalotarajiwa kufanyika kwenye ufukwe wa Cine Club, Kawe jijini Dar es Salam. Mratibu wa shindano hilo Peter Magambo, ameiambia mamapipiro blog kwamba alisema kwamba mbali na Diamond, shindano hilo pia litapambwa na burudani za aina mbalimbali zikiwemo toka kwa wanafunzo wa chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM) Alisema washindi kwa upande wa Miss IFM watashiriki shindano la Miss Higher Learning litakalofanyika baadaye mwaka huu ambapo warembo 12 watachuana kuwania taji hilo wakiwemo Suzana Siame, Speransia Tarimo, Agness Benard, Agness Goodluck, Phina Revocatus, Theresia Isaya, Jane Agostino, Rosa Damazo, Stella, Caroline Dandu, Fatina Francis na Leticia James. Magambo aliwataja washiriki watakaowania taji la Mr.IFM kuwa ni pamoja na Nicodemus Mahimbo, Fridoline Edward, Jumanne Kennedy, Derick Baraka, Godfrey Makinga, Josephat Mmassy, Phillip Japhet, Essae Mkindi, Saadat Saadat, Joshua Nkonmbugwa, Freeman Lutege na Livan Ehota.

Comments