MPIGANAJI RACHEL MWILIGWA ATANGULIA MBELE YA HAKI

Marehemu Rachel pichani katika moja ya sherehe za maadhimisho ya kuzaliwa kwake
Marehemu Rachel (kati)akiwa na wafanyakazi wewnzake wa kampuni ya New habari ambao pia wanaandika habari za michezo na burudani Mwani Nyangassa na Zaituni Kibwana. TASNIA ya habari nchini na hasa michezo na burudani imepata pigo baada ya mpiganaji wake, Rachel Mwiligwa ambaye alikuwa mhariri wa michezo wa gazeti la Mtanzania kufariki usiku wa kuamkia leo. Rachel alikuwa melazwa katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam tangu mapema wiki hii. Taarifa zaidi tutawaletea baadaye, ila hatuna budi kusema kazi yake mola haina makosa.

Comments