MICHUANO YA COPA COCA CIOLA KINONDONI YASHIKA KASI

Mchezaji wa Mickovila FC Richard Muya (kulia) akitafuta namna ya kumtoka mchezaji wa Sparrow FC Athumani Ndimbo wakati wa michuano ya Copa Coca-Cola ngazi ya wiliya iliyochezwa kwenye uwanja wa Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Sparrows ilishinda 2-1.


Na Mwandishi Wetu.
TIMU tatu za Wilaya ya Kinondoni jumamosi  zilijitupa uwanjani katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 yanayojulikana kama Copa Coca-Cola katika hatua ya ngazi ya wilaya , mechi hizo zilichezwa kwenye viwanja vya Tanganyika Peaks, Kawe, Dar es Salaam.
Mechi ya kwanza ilikuwa ni baina ya timu ya  A.B.C iliyoichapa timu ya Lugalo Boys magoli 3-2   huku magoli hayo yakiingizwa kinywani na wachezaji wake Julius Edward ambaye alifunga magoli mawili na Joseph Jacob aliyefunga goli moja.
Timu ya A.B.C ilionekana kutawala mchezo kuanzia kipindi cha kwanza hadi timu hizo zinakwenda mapumziko kwani timu hiyo iliweza kupata magoli mawili katika dakika ya 10 na ya 25  huku timu ya Lugalo Boys wakiwa hawajaona kitu.
 Magoli mawili ya Lugalo Boys yalifungwa kipindi cha pili kupitia wachezaji wake Emmanuel Michael na Benson Zengo dakika ya 50 na 80 huku A.B.C wakaongeza goli la tatu lililowafanya kutoka washindi katika mechi hiyo  dakika ya 85.
Katika mchezo mwingine uliochezwa kwenye viwanja hivyo  timu ya Sparows iliinyuka timu ya Mickovila magoli 2-1  ambapo magoli ya timu hiyo yaliwekwa kinywani na mshambuliaji wake Abdul Said katika dakika ya 25 na 50, huku goli la kufutia machozi la timu ya Mickovila likifungwa na Dickson Said dakika 43 ya mchezo huo.
Hata hivyo mechi hizo zilizochezwa katika viwanja hivyo zilimalizika kwa mchezo wa mwisho baina ya timu ya Makumbusho na Championi.Timu ya Makumbusho ilitoka kimasomaso kwa kuichapa Championi magoli 3-2.
Magoli ya timu ya Makumbusho yaliwekwa kinywani na wachezaji Kassimu Bokasa aliyefunga magoli mawili katika kipindi cha kwanza na cha pili cha mchezo huo huku goli la tatu likiwekwa kinywani na Omary Sudy. Hata hivyo Champion magoli yao mawili ambayo hayakuwawezesha kufika mbali yaliwekwa wavuni na mchezaji Hassan Abdalah.
Mwisho

Comments