MENEJA TWANGA PEPETA AJIUNGA MASHUJAA MUSICA


 Mshauri wa Mashujaa Musica King Dodoo kulia akizungumza na waandishi wa habari wakati wakimtambulisha meneja mpya wa bendi hiyo Martine Sospeter (kati) kushoto ni Rais wa Mashujaa musica, Chaz Baba.

ALIYEKUWA meneja wa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Martin Sospeter ametangaza kujiunga bendi ya Mashujaa Musica. 
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Martin alisema kwamba amejiunga Mashujaa Musica kwa ridhaa yake na wala si kwa lengo la kuidhoofisha au kuiua Twanga Pepeta, bali kuendeleza muziki wa dansi nchini. 
Alisema hana ugomvi na mkurugenzi wa Twanga Asha Baraka pamoja na kutangaza kuwa amemfukuza kazi wakati akiwa mkoani Mtwara na bendi yake  akimtuhumu kuihujumu bendi yake kitu ambacho hakina ukweli na  kimemuumiza sana kiasi cha kumtoa machozi.
 “juzi usiku nilishangazwa na kauli ya mkurugenzi wangu wa Asha Baraka ambaye namchukulia zaidi ya dada yangu akidai amenifukuza kazi kutokana kuhujumu bendi ikiwemo kushawishi wanamuziki kujiunga na bendi ya Mashujaa,  kauli ile ilinisikitisha sana kutokana na ukweli kwamba nilimuheshimu sana na kufanya naye kazi kwa  miaka 13 iweje hii leo aje anitolee maneno ya kunichafua katika vyombo vya habari,? 
“Sijawahi kuhusika na mpango wowote wa wasanii wa Twanga kuhamia Mashujaa na wala sikuwa nafahamu mpango huo zaidi ya kusikia fununu za chinichini na mwishowe wasanii hao kutangazwa kuhamia Mashujaa, hivyo napenda umma uelewe kwamba nimeondoka Twanga Pepeta na nimekabidhi kila kilichochao kama kuna kitu nadaiwa mtu alete uthibitisho,”alisema. 
Alisema ameshasaini mkataba wa kazi usio na mipaka, ambapo mbali na mkataba mnono, ameahidi kufanya kazi yake hiyo mpya kama ilivyokuwa Twanga ambapo alidumu nayo kwa muda mrefu na kuchangia kufika hadi hapo alipoachia, hivyo ameomba ushirikiano kwa uongozi, wanamuziki, Wadau na hata ninyi mwaandishi wa habari.

Comments