MCHUMA WA KHADIJA KOPA WAIBWA

GARI ya malkia wa taarab nchini Khadija Omary Kopa imeibwa hivi karibuni katika eneo la kulazia magari Mwananyamala B jijini Dar es Salaam.
Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam zinaeleza kuwa gari la Kopa aina ya Noah yenye rangui nyeusi la ufito wa fedha, ni minongoni mwa magari matatu yaliyoibwa katika eneo hilo na tayari taarifa zimelifikia jeshi la polisi ambalo linaendelea na uchunguzi.
Aidha, imeelezwa kuwa hgari jingine lililoibwa lilikuwa la msanii wa bongo fleva Dogo Hamidu ambapo walinzi wa eneo hilo walikimbia baada ya tukio.

Comments