MBONI MASIMBA AJA NA THE MBONI SHOW@EATV

 Mjasiriamali, mwanamitindo na mdau mkubwa wa michezo na burudani nchini Mboni Masimba (katika) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ujio wa Talk Show yake 'The Mboni Show' , kushoto ni mwongozaji wa show hiyo George Tyson na kulia ni mwakilishi wa EATV Sofia Mganya.
Dina aka Mamapipiro wakati wa hafla ya utambulisho wa 'The Mboni Show'

KIPINDI kipya cha runinga ‘The Mboni Show’ ambacho kitakuwa kikijadili masaula mbalimbali kinatarajiwa kuanza kurushwa katika kituo cha East Africa Televishen kuanzia Mei 31 mwaka huu.
mwandaaji wa kipindi hicho Mboni Masimba ameiambia mamapipiro blog kwamba kipindi hicho ambacho kitakuwa tofauti na vile vilivyozoeleka hapa nchini, kina lengo la kuburudisha, kuelimisha, kuonya na kuelekeza.
Alisema kipindi hicho kimegawanywa sehemu tano zikiwemo  ufunguzi, maswali kutoka kwa mtangazaji kwenda kwa wageni, maswali kutoka kwa hadhira kwenda kwa wageni, ‘My dreams come true’ na tamati.
“Kipindi kitakuwa kikihusisha wageni maalum ikishabihiana na mada husika kwa kipindi, huku pia ikialika hadhira ambayo itashiriki kwenye kuuliza maswali….lakini pia mgeni ambaye kipindi kitatimiza ndoto yake kwa kumzawadia haja ya moyo wake,” alisema.
Mboni ambaye pia ni mdau mkubwa wa muziki, mitindo na mjasiriamali aliongeza kuwa amedhamiria kuleta mapinduzi makubwa katika muendelezo wa vipindi vya mahojiano hapa nchini, hivyo amewataka wadau kukaa mkao wa kula.
Naye mwakilishi wa EATV Sofia Mganya alisema wameamua kupokea kipindi hicho kutokana na kukunwa na maudhui yake na kwamba The Mboni Show imetayarishwa na kampuni ya Chocolate Princes na kusimamiwa na George Tyson, itakuwa ikiruka kila alhamis kuazia saa tatu hadi saa nne usiku.

Comments