MAN CITY BINGWA ENGLAND

MABAO mawili ya dakika za majeruhi yameipa Manchester City ubingwa wa Ligi Kuu ya England, baada ya kuwafunga QPR waliocheza pungufu kwa muda mrefu. Pablo Zabaleta aliifungia City bao la kuongoza dakika ya 39 kabla ya makosa ya Joleon Lescott kumpa nafasi Djibril Cisse kuisawazishia QPR dakika ya 48. Joey Barton alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Carlos Tevez, lakini Jamie Mackie akaifungia bao la pili QPR dakika ya 66. Huku Manchester United ikiifunga Sunderland, City walionekana kupigana sana uwanjan na Edin Dzeko akasawazisha dakika ya 90 na Sergio Aguero akapiga la ushindi dakika ya sekunde chache baadaye. Hili ni taji la kwanza City tangu mwaka 1968, enzi hizo ligi hiyo ikiitwa Daraja la Kwanza.

Comments