MALAWI KUTUA ALHAMIS TAYARI KUIVAA STARS

TIMU ya Taifa ya Malawi inatarajiwa kutua Alhamis kwa ajili ya mchezo wa kimtaifa wa kirafiki dhidi ya Taifa Stars utakaopigwa Jumamosi kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi kwa Stars kwa ajili ya mchezo wake wa awali wa kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Angetile Osiah amesema kwamba Malawi itatua na msafara wa watu 27.
Aidha, kikosi cha Stars chini ya kocha wake Kim Poulsen kimepiga kambi kwenye hoteli ya Tansoma kikiendelea na mazoezi yake.

Comments