KOCHA WA AZAM FC AOMBA KAZI YANGA

ALIYEPATA kuwa kocha wa timu ya soka ya Azam FC Mbrazil Itamar Amourim ni miongoni mwa makocha 20 waliojitosa kuona kazi ya kukinoa kikosi cha Yanga.
Itamar ana makocha wengine wanaomba kazi hiyo kurithi mikoba ya Mserbia Kostadin papic aliyemaliza mkataba wake.
Katibu mkuu wa Yanga Mwesigwa Selestine amesema kwamba mbali na Itamar makocha wengine waliomba kazi wanatoka nchi za Ureno, Jamhurei ya Kidemokrasia ya Congo,Uholanzi, Ubelgiji, Ufaransa, Afrika Kusini, Uingereza na Australia. 

Comments