KIMENUKA JANGWANI, WANACHAMA WAVAMIA VURUGU TUPU

Makao makuu ya Yanga
WATU wanaosadikiwa kutumwa na wapinzani wa Mwenyekiti wa Yanga, Wakili Lloyd Bahargu Nchunga wamevamia makao makuu ya klabu, kuvuruga Mkutano wa Mwenyekiti huyo na Waandishi wa Habari mchana huu. Watu hao wanadaiwa kufanya vurugu zilizosababisha uharibifu makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam. Nchunga aliitisha mkutano na Waandishi wa Habari wa saa 5:00 asubuhi ya leo, kuelelezea yale yaliyofikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji jana. HIZI NI TAARIFA ZA AWALI, HABARI KAMILI INAKUJA

Comments