KIM AOMBA KUTOFANANISHWA NA POULSEN

KOCHA mpya wa timu soka ya Taifa 'Taifa Stars' Mdenmark Kim Poulsen amewataka wadau kutomfananisha na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Jan Poulsen. Kim ambaye alikuwa akizinoa timu za vujana, alipewa mikoba hiyo jana kutokana na kocha wa Stars mkataba wake kumalizika JUlai 30 huku Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likiamua kuachana naye. Akizungunza jijini Dar es Salaam jana, Poilsen alisema hayo ni majina tu lakini ufundishaji wake uko tofauti si na Poulsen tu bali hata makocha wengine wa ndani na nje ya nchi. Alisema kikubwakinachohitaji ni kupata ushirikiano wa kutosha toka TFF, wadau na hata wachezaji wa timu hiyo ili kuweza kutimiza malengo aliyoyaopanga ya kuhakikisgha timu hiyo inapata mafanikio makubwa. Poulsen ambaye amekuwa nchini kwa mwaka mmoja alisema anawafahamu wachezaji wa Tanzania hivyo hatopata shida katika kutekeleza majukumu yake hayo mapya. Aidha, Kim anatarajiwa kutangaza kikosi kipya cha Stars ambacho kitaingia nkambini kujiandaa na mchezo wake dhidi Ivory Coast utakaopigwa Juni 2 mwaka huu.

Comments