KIKOSI CHA SIMBA KUANIKWA DAR LIVE J'2, TUZO YA MAFISANGO KUTOLEWA

Klabu ya soka ya Simba inatarajiwa kufanya hafla maalum ya kujipongeza kwa ubingwa wake wa ligi kuu soka Tanzania Bara katika ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala jijini dar es Salaan Jumapili ya Mei 27 mwaka huu.
Kupitia hafla hiyo itakayohudhuiriwa na wadau mbalimbali, wanatarajiwa kutangaza kikosi cha wachezaji wapya waliosajili kwa ajili ya kuichezea klabu hiyo katika msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania Bara pamoja na michuano ya kimataifa.
Aidha, hafla hiyo itatumika pia kutangazwa kwa tuzo maalum ya kumuenzi kiugo wa timu hiyo Patrick Mutesa Mafisango aliyefariki wiki iliyopita kwa ajali ya gari jijini Dar es Salaam na kuzikwa jumatatu ya wiki hii nyumbani kwao Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Sherehe hizo zitapambwa na burudani kutoka kundi la Mashauzi Classic, bendi ya Msondo Ngoma, msanii wa bongo fleva Young D na wengineo.

Comments